Wakili Msomi

Ibara 49

Kiapo cha Makamu wa Rais

Serikali ya Jamhuri ya Muungano · Makamu wa Rais

Makamu wa Rais, kabla ya kushika madaraka yake ataapishwa mbele ya Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, kiapo cha uaminifu na pia kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.

Marejeo ya marekebisho: Sheria Na.34 ya 1994 ib.11

Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.