Wakili Msomi

Ibara 31

Ukiukaji wa Haki na uhuru

Jamhuri ya Muungano, Vyama vya Siasa, Watu na Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea · Haki na Wajibu Muhimu

(1)Mbali na masharti ya ibara ya 30(2), sheria yoyote iliyotungwa na Bunge haitakuwa haramu kwa sababu tu kwamba inawezesha hatua kuchukuliwa wakati wa hali ya hatari, au wakati wa hali ya kawaida kwa watu wanaoaminika kuwa wanafanya vitendo vinavyohatarisha au kudhuru usalama wa taifa, ambazo zinakiuka masharti ya ibara ya 14 na ya 15 za Katiba hii.

(2)Ni marufuku kwa hatua zilizotajwa katika ibara ndogo ya

(1)ya ibara hii kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria yoyote wakati wa hali ya hatari, au wakati wa hali ya kawaida kwa mtu yeyote, isipokuwa tu kwa kiasi ambacho ni lazima na halali kwa ajili ya kushughulikia hali iliyopo wakati wa hali ya hatari au wakati wa hali ya kawaida kushughulikia hali iliyosababishwa na mwenendo wa mtu anayehusika.

(3)Ifahamike kwamba masharti yaliyomo katika ibara hii hayataidhinisha mtu kunyang'anywa haki yake ya kuwa hai isipokuwa tu kwa kifo kama matokeo ya vitendo vya kivita.

(4)Kwa madhumuni ya ibara hii na ibara zifuatazo za Sehemu hii "wakati wa hali ya hatari" maana yake ni kipindi chochote ambapo Tangazo la Hali ya Hatari, lililotolewa na Rais kwa kutumia uwezo aliopewa katika ibara ya 32, linatumika.

Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 1984 Na.15 ib.6

Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.