Ibara 15
Haki ya uhuru wa mtu binafsi
Jamhuri ya Muungano, Vyama vya Siasa, Watu na Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea · Haki na Wajibu Muhimu
(1)Kila mtu anayo haki ya kuwa huru na kuishi kama mtu huru.
(2)Kwa madhumuni ya kuhifadhi haki ya mtu kuwa huru na kuishi kwa uhuru, itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kukamatwa, kufungwa, kufungiwa, kuwekwa kizuizini, kuhamishwa kwa nguvu au kunyang'anywa uhuru wake vinginevyo, isipokuwa tu-
(a)katika hali na kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria, au
(b)katika kutekeleza hukumu, amri au adhabu iliyotolewa na mahakama kutokana na shauri au na mtu kutiwa hatiani kwa kosa la jinai.
Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 1984 Na.15 ib.6
Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.