Wakili Msomi

Ibara 72

Watu wenye madaraka Serikalini kukoma utumishi wanapochaguliwa

Bunge la Jamhuri ya Muungano · Wabunge, Wilaya ya Uchaguzi na Uchaguzi wa Wabunge

Iwapo mtu yeyote mwenye madaraka katika utumishi wa Serikali, madaraka ya aina iliyotajwa katika ibara ya 67(2)(g) ataamua:-

(a)kuwa mgombea uchaguzi wa Rais au wa nafasi nyingine yoyote chini ya Katiba hii;

(b)kugombea uongozi wa ngazi yoyote katika chama cha siasa kinyume na masharti ya ajira, mtu huyo atahesabiwa kuwa utumishi wake umekoma tangu tarehe yake ya kuwa mgombea uchaguzi au ya kugombea uongozi katika chama cha siasa.

Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 1992 Na.4 ib.23 Sheria ya 1995 Na.12 ib.14

Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.