Wakili Msomi

Ibara 23

Haki ya kupata ujira wa haki

Jamhuri ya Muungano, Vyama vya Siasa, Watu na Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea · Haki na Wajibu Muhimu

(1)Kila mtu, bila ya kuwapo ubaguzi wa aina yoyote, anayo haki ya kupata ujira unaolingana na kazi yake, na watu wote wanaofanya kazi kulingana na uwezo wao watapata malipo kulingana na kiasi na sifa za kazi wanayoifanya.

(2)Kila mtu anayefanya kazi anastahili kupata malipo ya haki.

Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 1984 Na.15 ib.6

Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.