Ibara 11
Haki ya kufanya kazi, kupata elimu, na nyinginezo
Jamhuri ya Muungano, Vyama vya Siasa, Watu na Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea · Malengo Muhimu na Misingi ya Mwelekeo wa Shughuli za Serikali
(1)Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibu unaofaa kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa haki ya mtu kufanya kazi, haki ya kujipatia elimu na haki ya kupata msaada kutoka kwa jamii wakati wa uzee, maradhi au hali ya ulemavu, na katika hali nyinginezo za mtu kuwa hajiwezi. Na bila kuathiri haki hizo, Mamlaka ya Nchii itaweka utaratibu wa kuhakikisha kwamba kila mtu anaishi kwa jasho lake.
(2)Kila mtu anayo haki ya kujielimisha, na kila raia atakuwa huru kutafuta elimu katika fani anayopenda hadi kufikia upeo wowote kulingana na stahili na uwezo wake.
(3)Serikali itafanya jitihada kuhakikisha kwamba watu wote wanapata fursa sawa na za kutosha kuwawezesha kupata elimu na mafunzo ya ufundi katika ngazi zote za shule na vyuo vinginevyo vya mafunzo.
Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 1984 Na.15 ib.6
Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.