Wakili Msomi

Nyongeza ya Pili

Nyongeza ya Pili

ORODHA YA KWANZA

(Imetajwa katika ibara ya 98 (1)(a))

(Sheria ambazo mabadiliko yake yahitaji kuungwa mkono na heluthi mbili ya Wabunge wote).

Sura ya 500, Sheria ya kluthibitisha Tanganyika kuwa Jamhuri ya mwaka 1962: Ibara ya 3, 17,18, 23 na 26

Sura ya 508, Sheria ya Utumishi katika Idara ya Mahakama ya mwaka 1962: Ibara ya 22, 23, na 24

Sura ya 509, Sheria ya Utumishi Serikalini ya mwaka 1962: Ibara ya 22, 23, na 24.

Sura ya 512, Sheria ya Uraia, ya mwaka 1961: Sheria yote

Sura ya 557, Sheria ya Kuthibitisha Mapatano ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ya mwaka 1964: Sheria yote.

ORODHA YA PILI

(Imetajwa katika ibara 98 (1) (b)) Mambo ambayo mabadiliko yake yahitaji kuungwa mkono na theluthi mbili ya Wabunge wote kutoka Tanzania Bara na theluthi mbili ya Wabunge wote kutoka Tanzania Visiwani.

1. Kuwapo kwa Jamhuri ya Muungano.

2. Kuwapo kwa Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano.

3. Madaraka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

4. Kuwapo kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano.

5. Madaraka ya Serikali ya Zanzibar.

6. Mahakama Kuu ya Zanzibar.

7. Orodha ya Mambo ya Muungano.

8. Idadi ya Wabunge kutoka Zanzibar.

Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.