Nyongeza ya Kwanza
Mambo ya Muungano
(Imetajwa katika ibara ya 4)
1. Katiba ya Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
2. Mambo ya Nchi za Nje.
3. Ulinzi na Usalama.
4. Polisi.
5. Mamlaka juu ya mambo yanayohusika na hali ya hatari.
6. Uraia.
7. Uhamiaji.
8. Mikopo na baiashara ya Nchi za Nje.
9. Utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
10. Kodi ya Mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika, ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa nchini Tanzania unaosimamiwa na Idara ya Forodha.
11. Bandari, mambo yanayohusika na usafiri wa anga, posta na simu.
12. Mambo yote yanayohusika na sarafu na fedha kwa ajili ya malipo yote halali (pamoja na noti); mabenki (pamoja mabenki ya kuweka akiba) na shughuli zote za mabenki; fedha za kigeni na usimamizi juu ya mambo yanayohusika na fedha za kigeni.
13. Leseni ya viwanda na takwimu.
14. Elimu ya juu.
15. Maliasili ya mafuta, pamoja na mafuta yasiyochujwa ya motokaa na mafuata ya aina ya petroli na aina nyinginezo za mafuta au bidhaa, na gesi asilia.
16. Baraza la Taifa la Mitihani la Tanzania na mambo yote yanayohusika na kazi za Baraza hilo.
17. Usafiri na usafirishaji wa anga.
18. Utafiti.
19. Utafiti wa hali ya hewa.
20. Takwimu.
21. Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano.
22. Uandikishaji wa Vyama vya siasa na Mambo mengine yanayohusiana navyo.
Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.